Muro awaasa waandishi wa habari kuacha uwoga na kuendelea kusimamia ukweli.

Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Aliyekuwa Mtangazaji wa TBC1, Jerry Muro na wenzake 2, wameachiwa huru leo na hakimu Frank Mosha wa mahakama ya kisutu baada ya kuwaona hawana hatia na makosa waliyoshitakiwa nayo. Jerry na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matatu ya Kula njama ya kutenda kosa, kuomba rushwa na kujifanya maafisa wa Takukuru, madai ambayo yametupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.

Advertisements

Maswaada mpya wa sheria ni kichekesho hahahaha

Sasa mheshimiwa mbona unawakumbatia wakati walitoka nje? Tulia mama hawa ndiyo makamanda wenyewe wanajua kila kitu nyie mlikurupuka na kuleta ukada…Mimi sikutetei tena Bungeni nimekasirika sasa….. ngoja utaona mimi sindiyo mwenyewe? pale mjengoni?

Tamasha la Street University la funika Arusha

Eric Shigongo akitoa mada za ujasiriamali na
namna ya kujikomboa na umaskini kupitia biashara.
Tamasha kubwa la ujasiriamali la Street University lililofanyika kwa
kishindo ndani ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Jumapili
iliyopita, limeweka rekodi kwa kulifanya jiji hilo litingishike kwa
burudani kabambe kutoka kwa wasanii kibao waliokamua jukwaani pamoja
na mada motomoto za ujasiriamali zilizotolewa.

Risasi mchanganyiko lilikuwepo kwenye uwanja huo na kushuhudia jinsi
umati uliofurika, wakiwemo Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema na
askofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie walivyoyafurahia
mafunzo ya ujasiriamali na burudani ya kukata na shoka iliyoporomoshwa
na wasanii wa muziki wa injili na kizazi kipya Bongo, Christina
Shusho, Bonny Mwaitege, Abass Hamis Kinzasa ‘20%’ , Glorious Singers,
Dot Com Generation na Pastor Wambura.

“Tumepata mwitikio mkubwa kuliko hata tuliuvyotegemea. Tunawashukuru
sana wakazi wa Arusha na maeneo ya jirani kwa kutuunga mkono na
kujitokeza kwa wingi kusikiliza tulichowaandalia. Tunaamini maisha ya
wengi yatabadilika kwani tumepandikiza mbegu za ushindi na mafanikio
maishani.

“Tunawashukuru sana wadhamini waliowezesha kufanyika kwa tamasha letu,
Kampuni ya Global Publishers Ltd, Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa
Umma (PSPF), Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Wafanyabiashara na
Wakulima (TCCIA), Hoteli ya Kibo Palace ya jijini Arusha, Tripple A
Radio (88.5 FM), Sunrise Radio (94.8 FM), Mambo Jambo Radio (93.0 FM),
Sauti ya Injili Radio (92.2/96.2 FM)  na Radio 5 (105.7FM), zote za
jijini Arusha,” alisema Mwang’amba ambaye ndiye aliyekuwa mratibu wa
tamasha hilo.

posho si dhambi, dhambi ni posho inapokosa utu- LEMA

“POSHO SI DHAMBI , DHAMBI NI POSHO INAPOKOSA UTU” – LEMA

Nimetafakari sana niliposoma kwenye magazeti kuwa sisi wabunge tumeongezewa posho bila hata sisi kufahamu jambo hilo .
Na kila mtu ametoa maoni mbali mbali juu ya jambo hili , ni kweli ni msimamo wa chama chetu (Chadema) kupinga posho mbali mbali zisizokuwa na tija na tulikubaliana hivyo kwenye vikao vya Chama Chetu vya Wabunge na kupinga mfumo wa posho uliopo kwa sasa ni msingi sahihi wa Chama kuonyesha hisia na ubadhilifu mkubwa unaotokana na ulipwaji mbaya wa posho kama ambavyo imejitokeza mara nyingi na hata hivi karibuni tumeshuhudia madudu mengi kwenye ripoti ya kamati ndogo ya Bunge iliyomchunguza Jairo. Lakini suala hili haliwezi kuepukwa kabisa na Chama kinajua ila utaritibu wa ulipwaji posho kwa watumishi mbali mbali wa umma ni tatizo kubwa na kuna mapungufu mengi sana ndio maana kupinga posho haina maana tu ya kupinga kiwango cha pesa anachopokea Mbunge au mtumishi yeyote wa UMMA bali mfumo mzima wa sera ya posho ili uweze kuwa na tija na kupunguza mianya ya wizi katika mfumo huu ambao umekuwa ukitumika vibaya kuliibia Taifa.

Pengine sisi wabunge ni vyema tukatambua kwanini wananchi wanapiga kelele kuhusu posho nilishawahi kusema Bungeni wakati nachangia kwenye Wizara ya Ustawi wa Jamii kuwa mshahara wa Wabunge , posho mbali mbali za Wabunge pamoja na marupurupu mengine yanaonekana kuwa anasa pale watumishi wengine wa serikali kama Manesi ,Asikari Magereza,Polisi ,Makarani Mahakamani wanapolipwa chini ya shilingi laki mbili na nusu kwa mwezi na wakati huo huo wanasikia mwakilishi wao akipiga kelele Bungeni kuwa posho ya laki mbili kwa siku ni ndogo. Ndio maana nimesema “POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU , Na hapa lazima kutokee ugomvi wa kimasilahi na mgogoro mkubwa kati ya mwakilishi na anaye wakilishwa.

Pengine masilahi anayopata Mbunge ni ya kawaida sana tena sana ila yanaonekana kuwa anasa pale ambapo yeye kama mwakilishi anapolipwa kiwango cha posho cha siku moja ambacho ni sawa na mshahara wa mpiga kura wake kwa siku thelasini. Mimi nafikiri namna peke ya wabunge kutetea masilahi yao bora kwanza ni kupigania masilahi ya wapiga kura wote Tanzania na tukifanya hivi kama Wabunge hakuna Mwananchi hatakayeshangaa kwanini Mbunge awe na masilahi bora kwani ubunge ni nafasi kubwa pia inayositahili heshima kubwa kwani ni uwakilishi katika jamii.

Ebu jiulize wananchi wanaposikia Wabunge wamepewa milioni tisini kununua magari na wakati huo huo serikali imenunua bajaji kuwa ndio magari ya kubeba wakinamama wajawazito yaani (Ambulance) ni wazi kabisa wabunge wataonekani ni watu katili na walioenda bungeni kwa masilahi binafsi japo kuwa ukweli unabaki kuwa Wabunge wanahitaji magari imara na mazuri. Lakini Wabunge kama watafikiri Bajaj ni sawa kuwa gari la wakinamama wajawazito na wao kuchukua milioni tisini kwa magari ya binafsi bila kupiga kelele na kukataa unyanyasaji huu kwa wakina mama na Wagojwa ,hivyo ni dhahiri kuwa ugomvi hapa katika posho na masilahi ya Wabunge utasababishwa na tofauti ya masilahi dhidi ya wale waliowachagua kuwatetea ,Hivyo namna pekee Mbunge anaweza kutetea masilahi yake bora bila kuingiliwa na na kubugudhiwa ni Mbunge kuanza kufikiria masilahi ya watu wengine ambao pia ni watumishi wa UMMA ambapo yeye ni mwakilishi wake .

Nafahamu kuwa pamoja na kupinga mfumo mzima wa utaritibu wa posho ulivyo sasa tafakari ya kweli ni kwamba masilahi ya watumishi wa UMMA bado ni madogo sana kwa hiyo Uzalendo wa kweli sio tu kupinga masilahi bora bali serikali iwajibike kikamilifu kudhibiti wizi na ufisadi unaotokana na utaritibu mbaya wa ulipwaji posho , kuongeza makusanyo katika kodi mbali mbali ,kutumia rasilimali za Nchi vizuri ili masilahi ya watu wote Nchi hii yaweze kuwa na tija kwa maisha ya Watanzania na watu wengi waweze kuishi maisha ya faraja na kutimiza malengo yao muhimu ya maisha
Ndio maana nimesema “POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.

Nitakuwa ni mtu mwenye mashaka sana kama nikiwaza kuwa masilahi duni na maisha ya kuishi chini ya kiwango ni Uzalendo , Sasa Wabunge mkitaka msipigwe mawe barabarani ,msitukanwe , msionekane ni wasaliti wa jamii aliyowachagua , Sasa huu ni wakati wakusema , Mshahara wa Polisi ,Magereza,JWTZ, Walimu, Makarani Mahakamani na hata sekta zote za Serikali na Binafsi masilahi ya mishahara yao yaongezwe kwa asilimia kama ambavyo mmjiongozea nyie kwenye posho zenu tena zinazohusu siku moja tu lakini wao wanaomba kwa mwezi lakini hawapati. Sasa pamoja na kupinga mfumo mzima wa sera ya posho kama ambavyo Mwenyekiti wetu wa Taifa alisisitiza na kuomba sera hii iangaliwe upya ili kupunguzia Taifa mzigo mkubwa na kuboresha viwango vya mishahara vya watumishi wa UMMA , ni vyema nikarudia kusema kuwa ““POSHO SIO DHAMBI ILA POSHO NI DHAMBI PALE POSHO INAPOKOSA UTU.

Ni kweli gharama za Maisha zimepanda lakini hazikupanda kwa Wabunge tu pia kwa Wananchi wote wanaoishi Tanzania , Hivyo tukiacha ubinafsi tukawajibika vizuri Bungeni kulinda masilahi ya Taifa na kutetea maisha ya Wananchi wetu, bila shaka hata tukionekana tunaendesha magari ya kifahari kama Rolls Royce, Bentley, Benz , hakuna mwananchi hatakeyesema kwa nini Mbunge anaendesha gari zuri kwani kila mtu atakuwa na afadhali ya maisha ktk Nchi yetu.

“ Baba yangu aliniambia “ Watu wengi wanaokwenda Kanisani na Misikitini huwa wanatoa sadaka ndogo kuliko pesa wanayotumia sehemu mbali mbali za anasa ndio maana Taifa lina Bar nyingi kuliko nyumba za Ibada” TAFAKARI

LEMA- M

Waraka wa Lema wawatia vijana ujasiri na moyo, kulitumikia taifa lao hata kwa mateso

JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA 

UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU. 

Wapendwa wapiga kura wangu na Watanzania wenzangu. 

Sina wakati mgumu kuchukua maamuzi haya yanayotokea leo. Upendo huu nilio nao 

kwa watu wa Arusha na nchi yangu ni sababu ya msingi ya maamuzi haya. Nimetishwa 

mara nyingi, rafiki zangu wametishwa, jamii ya watu duni imeendelea kuishi kwa 

mashaka na matisho kwa muda mrefu. 

Katika mazingira haya, nikawaza sana kuwa anatakiwa kutokea mtu mmoja jasiri 

atakayeweza kuona thamani ya watu wengine. Huyo mtu anaweza kuwa wewe lakini 

kwa wakati huu siwezi kumsubiri tena na nimechagua kuwa mimi nikiamini kuwa 

utanikuta nikiendelea na safari ya ukombozi. Tupo wengi sana tunaotaka mabadiliko, 

haki na ukweli. Hata hivyo hofu, woga na mashaka yamepoteza thamani yetu yote ya 

maana ya kuishi . 

Waliofungwa kwa kuonewa na kuteswa, waliokosa chakula na kulala nje, waliokwenda 

hospitali na kukosa madawa, waliokosa ajira na kipato mpaka kujikuta wametoroka 

familia zao, waliopoteza matumaini ya maisha, waliopora utajiri wa nchi yetu kwa 

manufaa yao binafsi, walionunua haki na sheria dhidi ya wajane na wanyonge na 

kuwapora vipato vyao vidogo na mashamba yao, USIULIZE SABABU NINI!. 

Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati 

wajane na wanyonge wanaonewa. 

NIliposikia wengine wanaandamana kupinga uovu, uonevu, wizi, ufisadi na ukandamizaji 

wa haki nikasema ni hao na wala sio mimi, kumbe nilipaswa kuwa mbele katika harakati 

hizi. 

Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata 

taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani 

wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, 

nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya 

biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI, dhahabu zetu, almasi yetu, 

Milima na mabonde yetu, Tanzaninte yetu, samaki wetu, Uranium yetu, makaa ya mawe 

yetu, utalii wetu, ardhi na kilimo chetu na zaidi utu na mahusiano yetu. 

 Na sasa siwezi kukaa kimya tena. NI afadhali vita inayotafuta haki na usawa kuliko amani 

inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu. Na katika msingi huu hofu na 

mashaka vimekosa thamani kwangu, sitamwogopa mtu yoyote, mwenye silaha yoyote, 

mwenye cheo chochote na wala sitaogopa jela yoyote katika kupigania haki, utu wa 

kweli katika jamii yangu. Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela 

na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasa 

bila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI 

TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU. 

Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA 

KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ,” JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA 

KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA 

BINADAMU. 

Kila mara nilipotishiwa nikagundua wanaonitishia, wananitishia kwa jela na mauti. Na 

mimi nikagundua na nikatambua ni afadhali kuishi miaka hamsini jela huku sababu ikiwa 

ni kupinga uonevu na ukandamizaji kuliko maisha ya woga na anasa yasiyo na kusudi 

katika kutetea utu na heshima ya mwanadamu mwenzangu. 

Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki 

msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu. 

Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, 

watakaotupongeza na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni 

mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema. MSIOGOPE, 

MSIOGOPE, MSIOGOPE , MUNGU YUPO UPANDE WETU. 

Mhe Godbless Lema (MB) – Arusha Mjini 

31 Oktoba 2011.

Kilewo: alaani serikali kwa kuwaongezea wabunge posho.

Haya ni maneno ya Kilewo alipokuwa anatoa msimamo wake kuhusu wabunge kuongezewa posho. Natafuta neno zaidi ya ukichaa lakini silipati: yaani Tumeshindwa kulipa madeni ya wazee, tumeshindwa kutoa mikopo kwenye vyuo vya elimu ya juu, tumeshindwa kuzibiti ongezeko la watoto wa mitaani, tumeshindwa kutoa ajira kwa vijana, Tumeshindwa kuwapatia wanafunzi wa shule za msingi japo mlo mmoja kwa siku, kwa kigezo cha serikali haina fedha….. Hii ni dharau kubwa sana kwa wabunge kuongezewa posho wakati kuna wafanyakaziwa muhimu kuliko wabunge, Walimu, madaktari, police, hawa nao vipi? Acheni kucheza na kodi za Watanzania kwakutaka kuwanyamazisha wabunge. Watanzania Tuungane kwa pamoja katika kupinga unyonyaji huu wa kihuni kabisa

Kilewo awashukuru mabalozi waliyojitokeza kuwasaidia Vijana wa Kitanzania.

UPDATE
Ndugu zangu Watanzania: Siku ya jana Tar 27/11/2011 ilikuwa siku kubwa sana kwangu na siku ya kumbukumbu kwangu…. Nimefanikiwa kukutana na watanzania wenzangu na kuweza kujadili mambo ya msingi sana yanayo husu jamii ya kwetu ya kitanzania. Tlijadili Agenda mbili. 1. watoto wa mitaani. 2. Makahaba. kikao tulikiarisha mpaka j2 ya wiki ijayo ya Tar 3/12/2011 kikao kilifanyikia Grandvilla hotel na kijacho kitafanyikia GRANDVILLA HOTEL. Shukurani kwa wote waliyofika.. mungu awabariki sana.

Ndugu zangu Watanzania: Nimekaa chini nakutafakari sana juu ya utu wa mwanadamu ni kagundua kunamakosa nilikuwa nikiyafanya eidha kwakutokujua ama kwa makusudi: Nimeadhimia ya fuatayo kuhusu maisha ya watoto wa mtaani na dada zetu wanaojiuza kwa hali mbaya ya maisha.

1. sinto kula wa kulala bila kuwezesha watoto wa 5 kwa wiki na dada mmoja kutoka kwenye maisha waliyo nayo sasa kwenda kwenye maisha mapya.
2. Sina haja ya kuwa kiongozi tena kama nitashindwa kuokoa vijana wenzangu kula madawa ya kulevia na kupoteza nguvu kazi ya taifa. Mungu naomba unisaidie kulisimamia hili.

Ndugu zangu kila j2 nitakuwa na kikao jinsi ya kuwasaidia watanzania hawa wenzetu ambao wanahitaji msaada wa kiakili na faraja iliwaweze kurudi kwenye hali zao za kawaida kulitumikia taifa lao, Watu hawa lazima washiriki kwenye mchakato mzima wa kulijenga taifa lao.

Ningependa kukutana na watanzania wenzangu wazalendo kwenye ofisi za chama mkoa wa kinondoni (chadema) zilizopo Mwananyamala. Kwa ambao watahitaji kuelekezwa ofisi zilipo mawasiliano 0714-225960 muda ni saa kumi jioni. Mungu awabariki sana kwa kuwa na mioyo ya upendo.

kilewo: ashiriki mazishi ya mwalimu wake wa shule ya msingi Lwami

Katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum ya Dar es salaam, Bwana Kilewo akiwa na wakazi wa Wilaya ya Mwanga kwenye Msiba wa Mwalimu wake wa shule ya msingi Lwami iliyopo kwenye kitongoji cha Lwami Tarafa ya Mwanga. Kilewo amesema alikuja Mwanga kwaajili ya mikutano ya chama na vikao vya ndani vya Chama ila baada ya kupata Taarifa ya Msiba huwo ameamua kukatiza ziara yake na kuungana na Ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu kwenye msiba huwo, Mwalimu alinifundhsha Somo la kiingereza Darasa la Tano… cha msingi hapa ni kumuombea kwa mungu maana leo ametangulia nasisi tutafuata. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.amen

CHADEMA YA JIBU CCM KITAALAM ZAIDI.

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
KURUGENZI YA HABARI NA UENEZI –MAKAO MAKUU
TAMKO KWA UMMA WA WATANZANIA

YAH: KAMATI KUU YA CCM KUMWAGIZA RAIS KIKWETE AKUTANE NA VYAMA VINGINE VYA SIASA

Kurugenzi ya Habari na Uenezi imeshangazwa na tamko lililotolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye kuwa “Kamati Kuu ya CCM imemwagiza Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete akutane na vyama vyote vya siasa badala ya CHADEMA peke yake” aliendelea Kusema kuwa …… “Pamoja na kukubali akutane na CHADEMA, tumetahadharisha kuwa lazima kushirikisha wajumbe wengine kutoka kwenye vyama vyenye uwakilishi ndani ya Bunge isiwe CHADEMA pekee”.

Awali ya yote tunapenda kusisitiza kuwa maridhiano ya kitaifa juu ya mchakato wa kuweza kufikia kupata katiba mpya ni suala ambalo ni la muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu na haswa kama muafaka huo utafikiwa kwa nia njema ya kujenga na kuimarisha mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali dini, rangi, kabila ama itikadi za vyama vyao.

Tamko la Kamati Kuu ya CCM linaonyesha muendelezo wa matamko ambayo wamekuwa wakiyatoa kila mara wanapokutana, mathalani kikao kilichopita kiliiagiza serikali kuwa bei ya mafuta ya taa lazima ishuke, kitu ambacho mpaka leo hakijafanyiwa kazi na hii inaonyesha jinsi ambavyo Kamati kuu hiyo isivyokuwa na msimamo juu ya maamuzi yake na maagizo yake inayotoa kwa viongozi wa kiserikali.

Tamko hili, limetushangaza kwani limeonyesha wazi kuwa kuna hofu miongoni mwa viongozi na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kuwa sheria iliyopitishwa na wabunge wa CCM kwa kushirikiana na wale wa CUF haina muafaka wa kitaifa na hivyo wanamwagiza Rais kukutana na makundi mengine ili kupata maoni kabla ya kuisaini sheria hiyo.

CHADEMA tuliandika barua kwa Rais naye alikubali kukutana nasi, kitendo cha Kamati Kuu ya CCM kutoa tamko hili ni dhahiri kuwa kamati kuu ya CCM imejitwalia madaraka ya kuwa wasemaji wa vyama vingine vyenye uwakilishi Bungeni ambao mpaka leo hatujawasikia wakitoa tamko juu ya suala hilo. Tunajiuliza hivi Kamati Kuu ya CCM leo imekuwa ndio wasemaji wa vyama vyenye uwakilishi Bungeni ukiiondoa CHADEMA?

Pili, Vyama vyenye uwakilishi Bungeni ukiiondoa CHADEMA NA NCCR-Mageuzi waliopinga muswada huu, vyama vingine mathalani CUF, CCM na TLP wao waliunga mkono kupitishwa kwa muswada huu, sasa Kamati Kuu ya CCM inataka wakakutane na Rais ili kujadili kitu gani? Wakati walikuwa ni sehemu ya maamuzi ambayo CHADEMA na wadau mbalimbali wanayalalamikia na ndio maana tukataka kuwasilisha malalamiko yetu kwa Rais.

Tunapenda kuikumbusha Kamati Kuu ya CCM kuwa CHADEMA iliomba kukutana na Rais wa Nchi na sio kama Mwenyekiti wa chama, iwapo Rais atakubaliana na agizo hili la Kamati Kuu ya CCM itakuwa dhahiri kuwa ni muendelezo wa ushahidi kuwa viongozi wa Kiserikali wamekuwa wakitimiza majukumu yao kutokana na shinikizo la Chama hata kwenye masuala ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu kama suala hili la Katiba lilivyo.

Mwisho, Tungependa kumshauri Rais kuwa pamoja na kukutana na CHADEMA atenge muda ili aweze kukutana na makundi mengine mbalimbali ya kijamii yenye maoni na malalamiko kabla ya kusaini sheria iliyopitishwa na Bunge kwa maslahi ya taifa letu na ili kuweza kuleta utengamano wa kitaifa .

Imetolewa na

……………………
Erasto Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
24 Novemba 2011.